ALIYEKUWA MENEJA WA TIMU YA TUSKER FC NEVILLE PUDO, AMEAMUA
KUCHUKUA MAPUMZIKO NA KUACHANA NA MASUALA YA UTAWALA WA SOKA.
KULINGANA NA PUDO, AMBAYE AMEKUWA KIONGOZI WA KLABU HIYO KWA MUDA
MREFU, KWA SASA HATOKIMBILIA WADHIFA MWINGINE KATIKA KLABU YOYOTE, BALI
ITAMCHUKUA MUDA KATIKA KUFANYA MAAMUZI.
HATA HIVYO, MENEJA HUYO AMESEMA HATOKACHA MILELE PASIPO
KUREJEA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA, ILA JAMBO HILO SI LA HIVI KARIBUNI.
TIMU YA TUSKER INAKAMATA NAFASI YA PILI KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU
SOKA KENYA WAKIWA NA ALAMA 39, POINT TANO NYUMA YA VINARA WA LIGI HIYO AFC
LEOPARDS, WALIO NA POINT MOJA MBELE YA SOFAPAKA WANOSHIKILIA NAFASI YA TATU WAKIWA NA AKIBA YA MCHEZO MMOJA.
TUSKER FC WATAKUWA NA KIBARUA KINGINE JUMATATU AGOST 27, DHIDI
YA MABINGWA WA 2010, TIMU YA ULINZI STARS, MCHEZO UTAKAOPIGWA KATIKA DIMBA LA
NYAYO MAJIRA YA SAA MOJA USIKU.
No comments:
Post a Comment