KOCHA WA MALI PATRICE CARTERON JUMATANO HII ALIKUWA
SAINT ETIENNE NCHINI UFARANSA, AKIFUATILIA MAZOEZI YA MCHEZAJI BAKARY SAKO
MWENYE UMRI WA MIAKA 24, KUNAKO KITUO CHA ETRAT, AMBAPO MWAKA 201O MCHEZAJI
HUYO ALIFANYA VIZURI KATIKA LIGI ONE NCHINI HUMO.
SAKO NI MZALIWA WA UFARANSA, JAPO WAZAZI WAKE NI RAIA WA
MALI, KWANI ANAMILIKI HATI YA KUSAFIRIA YA UFARANSA NA AMEKICHEZEA KIKOSI CHA
TIMU YA VIJANA WA NCHI HIYO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 21, NA HIVI SASA
ANAJIWINDA KUJIUNGA NA TIMU YA WAKUBWA.
KOCHA CARTERON NIA NA MADHUMUNI YA SAFARI YAKE ILIUKUWA NI
KUMSHAWISHI MCHEZAJI HUYO KUREJEA KUKIPIGA NA TIMU YA TAIFA YA MALI, LAKINI
MAZUNGUMZO YALIYOFANYIKA BAINA YA PANDE MBILI HIZO BADO YANASUBIRI UAMUZI WA
MCHEZAJI MWENYEWE.
TIMU YA TAIFA YA MALI ITACHEZA NA BOTSWANA MCHEZO WAKE WA
KWANZA MJINI BAMAKO MAPEMA MWEZI WA TISA KUTAFUTA TIKETI YA KUSHIRIKI MICHUANO
YA AFCON 2013.
No comments:
Post a Comment