September 26, 2014

11 WA BAFANA BAFANA DHIDI YA KONGO BRAZAVILLE




Kocha wa Bafana Bafana Ephraim Mashaba ametangaza kikosi kitakachokabiliana na Congo Brazzaville kwenye mchezo wa kuwania AFCON 2015 utakaopigwa mwezi ujao.
Kikosi hicho kimetangazwa katika makao makuu ya ofisi za chama cha soka nchini humo zilizo mjini Johannesburg hii leo.
Mashaba na kikosi chake watasafiri kwa mara ya kwanza kuelekea mjini Pointe Noire Brazzaville kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa October 11 na kurudiana na Congo October 15 mjini Polokwane.
Bafana Bafana inakamata nafasi ya pili mwa A, nyuma ya Congo baada kushinda bao 3-0 dhidi ya Sudan na kutoka sare tasa na Nigeria mjini Cape Town mwezi uliopita.
Kikosi cha Bafana Bafana:
Makipa:                   

Senzo Meyiwa, Darren Keet, Duimisani Msibi
Mabeki:
Anele Ngcongca, Ayabulela Magqwaka, Sibusiso Khumalo, Thulani Hlatshwayo, Kwanda Mngonyama, Erick Mathoho, Thabo Matlaba, Rivaldo Coetzee, Tefu Mashamaite
Viungo:
Themba Zwane, Sibusiso Vilakazi, Oupa Manyisa, Andile Jali, Dean Furman, Thulani Serero, Mandla Masango, Keagan Dolly, Reneilwe Letsholonyane,
Washambuliaji:  
Tokelo Rantie, Bongani Ndulula, Kermit Erasmus, Fagrie Lakay

BENTEKE KURUDI UWANJANI HIVI KARIBUNI






Bosi wa Villa Paul Lambert ameweka wazi kuwa mshambuliaji wake Christian Benteke huenda akajumuika kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Manchester City  October 4.
Benteke aligonga vichwa vya habari nchini Uigereza kufuatia kufunga magoli 23 katika mashindano yote kwa mara ya kwanza akiichezea Villa, na licha ya kukabiliwa na majeruhi msimu uliopita, lakini alifunga magoli 11.
Kurudi kwake uwanjani kutaongeza ari ya kikosi cha Villa na kocha Lambert anasema Benteke anaendelea vizuri, na tamtumia lakini kwa tahadhari kubwa.
Villa inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya kufanikiwa kushinda mechi tatu mfululizo katika michezo mitano ambayo timu hiyo imekwishacheza.

August 28, 2012

TUZO YA (SOYA) KUZINDULIWA JUMATANO JIJINI NAIROBI


TOLEO LA 2012 LA TUZO YA MWANAMICHEZO BORA WA MWAKA WA KENYA, AL MAARUFU (SOYA) LITAZINDULIWA JUMATANO ASUBUHI MJINI NAIROBI.

SHEREHE ZA UZINDUZI HUO ZITAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MICHAEL JOSEPH MJINI NAIROBI NA KUHUDHURIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA SAFARICOM, BOB COLLYMOREATAKAEMABATANA NA MMOJA WA WAANZILISHI WA TUZO HIYO NA MWENYEKITI PAULO TERGAT, KUBARIKI SHUGHULI HIYO, ITAKAYOANZA SAA SITA MCHANA.

EGYPT OPEN GATES FOR ZAMALEK FANS


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA MISRI IMETOA IDHINI KWA ZAMALEK KURUHUSU MASHABIKI WAO  KURUDI UWANJANI KATIKA MECHI INAYOFUATA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA DHIDI YA CHELSEA YA GHANA.

KWA MUJJIBU WA SUPERSPORT.COM TAARIFA ZINASEMA KWAMBA WIZARA YA MAMBO YA NDANI IMETOA AGIZO HILO RASMI KWA MAAFISA WA ZAMALEK.

HATA HIVYO MKURUGENZI WA ZAMALEK ALAA MEKLED AMEIAMBIA SUPERSPORT.COM KWAMBA MASHABIKI WAPATAO ELFU TATU WATAPATA FURSA YA KUHUDHURIA MCHEZO UTAKAOFANYIKA KWENYE UWANJA WA ACADEMY YA JESHI.

ZAMALEK WAKIWA BILA POINTI HATA MOJA BAADA YA KUPOKWA POINT NA CAF, WATAKUWA WENYEJI WA CHELSEA YA GHANA SEPTEMBA MOSI, WAKATI BEREKUM CHELSEA AMBAO WANA POINTI TANO WAKIWA NA HAJA YA KUSHINDA NA KUCHEZA KATIKA HATUA YA NUSU FAINALI.

EAGLE WINGS RETURN HOME WITH REGIONAL TITLE


KAMA WALIVYOAHIDI TOKA AWALI, MABINGWA WA KIKAPU NCHINI KENYA, TIMU YA WANAWAKE YA EAGLE WINGS JANA USIKU IMEREJEA NYUMBANI KIFUA MBELE, BAADA YA KUWATANDIKA NDUGU ZAO TIMU YA MAMLAKA YA BANDARI (KPA) NA KUTWAA TAJI LA MICHUANO YA KIKAPU YA KANDA YA TANO KWA MWAKA 2012.

WAKIWA NA KOMBE HILO, EAGLE WINGS SASA WAMEPATA TIKETI YA KUWA TIMU PEKEE KUTOKA KENYA ITAKAYOWAKILISHA KWENYE MASHINDANO YA VILABU BINGWA AFRICA, FIBA  YATAKAYOFANYIKA NCHINI IVORY COAST BAADAYE MWEZI OKTOBA.

EAGLE WINGS ILIWABWAGA WAPINZANI WAO WA JADI KPA, KATIKA FAINALI ILIOPIGWA LUGOGO MJINI KAMPALA KWA USHINDI WA VIKAPU 77-54 BAADA YA KUONGOZA KWA ALAMA 31-30 ZA KPA MPAKA HALF TIME.