August 24, 2012

WAKENYA WAFANYA VIZURI DIAMOND LEAGUE




BAADA YA KUMALIZA VIBAYA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI 2012 JIJINI LONDON, MKENYA PAMELA JELIMO, HAPO JANA, AMEIBUKA KIDEDEA KATIKA MBIO ZA DIAMOND LIGI MJINI LAUSANNE NA KUMPIGA BAO MSHINDI WA MEDALI YA DHAHABU MRUSI MARIYA SAVINOVA AKITUMIA MUDA WA SAA 1:57:59, AKIMUACHA KWA UMBALI WA MITA 20.

KWA UPANDE WA WANAUME MBIO ZA MITA 1500, SILAS KIPLAGAT ALIEMALIZA WA SABA MJINI LONDON, AMESHINDA MBIO HIZO AKITUMIA MUDA WA SAA 3:31.78 NA KUMPIKU MKIMBIAJAI WA ETHIOPIA GEBREMEDHIN ALIEKAMATA NAFASI YA PILI.

WAKATI HUO HUO, MFUKUZA YOHAN BLAKES AMEUDHIHIRISHIA UMMA WA RIADHA NCHINI JAMAICA KUWA ANAWEZA KUFANYA VIZURI PASIPO UWEPO WA MKIMBAJI MWENZA USAIN BOLT, BAADA YA KUWEKA REKODI YA KUWA MKIMBIAJI WA PILI KATIKA HISTORIA YA MBIO ZA MITA 100, AKITUMIA MUDA WA SEKUNDE (9.69) NA KUMUACHA MKONGWE TOKA MAREKANI TYSON GAY ALIEMALIZA KWA SEKUNDE (9.83) HUKU NAFASI YA TATU IKIKAMATWA NA MJAMAICA NESTA CARTER AKITUMIA MUDA WA SEKUNDE 9.95.

NA KATIKA MBIO ZA MITA 200 USAIN BOLT ALISHINDA MBIO HIZO KIRAHISI AKITUMIA MUDA WA 19.58.


see more @www.michezoafrika.com

No comments:

Post a Comment