MABINGWA WA KIKAPU WA KENYA, TIMU YA EAGLE WINGS MAPEMA LEO
IMEDHIRISHA UBABE WAKE BAADA YA KUITUNGUA TIMU YA DON BOSCO YA TANZANIA VIKAPU
92 – 36 KATIKA MICHUANO YA AWALI YA MASHINDANO YA KANDA YA TANO YANAOENDELEA
KWENYE UWANJA WA LUGOGO MJINI KAMPALA.
KULIKUWA NA TIMU TATU TU
KATIKA MZUNGUKO HUO KUFUATIA KLABU YA APR YA RWANDA KUJITOA
MASHINDANONI.
SIKU YA JUMATATU AUGUST 20, TIMU YA EAGLE WINGS ILIICHAPA UGANDA CHRISTIAN
UNIVERSITY VIKAPU 75-64 KATIKA
MECHI YAO YA KWANZA.
KWA MATOKEO HAYO, TIMU YA KENYA SASA
IMEPENYA NA KUINGIA NUSU FAINALI YA MASHINDANO
YA MIKOA NA WATACHEZA WASHINDI WA PILI KATIKA
KUNDI A AMBAO NI MAMLAKA YA BANDARI, NUSU FAINALI YA MASHINDANO HAYO ITAPIGWA
JUMAMOSI YA WIKI HII.
ROSE OUMA
KWA MARA NYINGINE TENA ALIIBUKA MFUNGAJI
BORA KATIKA MCHEZO DHIDI YA DON BOSCO AKIWA NA POINTI 21. SUSAN AKINYI
PAMOJA NA MCHEZAJI MUHIMU (MVP) WA LIGI KUU YA KIKAPU KENYA, SAMBA
MJOMBA WOTE WAMEPATA
POINTI 17, HUKU KWA UPANDE WA DON
BOSCO YA TANZANIA MCHEZAJI SAIDA MOHAMMED NDO AMEIBUKA MFUNGAJI
BORA AKIWA NA POINTI 8.
see more... @michezoafrika.com
No comments:
Post a Comment