BAADA YA HIVI KARIBUNI NCHINI IVORY COAST KUIBUKA
MASHAMBULIZI YA RISASI DHIDI YA WANAJESHI WA NCHI HIYO, SHIRIKISHO LA SOKA LA
SENEGAL (FSF) LIMEPANGA KUOMBA
KUBADILISHIWA UWANJA KWA TIMU ZOTE, UTAKAOTUMIKA KWA MCHEZO WA KUWANIA
TIKETI YA AFCON 2013 ULIOPANGWA KUCHEZWA ABIDJAN TAREHE 8, MWEZI WA TISA
UTAKAOWAKUTANISHA WENYEJI IVORY COAST NA SENEGAL.
RAIS WA SHIRIKISHO HILO LA SOKA SENEGAL, AUGUSTIN SENGHOR,
AMESEMA KAMA HALI HIYO ITAENDELEA, WATALAZIMIKA KUPIGA HODI KATIKA SHIRIKISHO
LA SOKA BARANI AFRICA (CAF) NA KUOMBA MCHEZO HUO UCHEZWE KATIKA NCHI ZA JIRANI
KWA USALAMA WA WACHEZAJI WAKE.
WATU WASIOJULIKANA WENYE SILAHA, WIKI
MBILI ZILIZOPITA WALIIBUA MASHAMBULIZI MFULULIZO DHIDI
YA MAKAMBI YA KIJESHI,
VITUO VYA POLISI NA VITUO VYA UKAGUZI
MJINI ABIDJAN NA KATIKA
MIJI MINGINE, NA KUUA WATU TAKRIBANI 15, NA KUBOMOA MAGEREZA NA
MAHABUSU KUTOWEKA HURU KOSIKOJULIKANA.
HATA
HIVYO, WIZARA YA ULINZI YA IVORY COAST IMEIUTHIBITISHIA UMMA KUWA HALI HIYO IKO CHINI
YA UDHIBITI NA IMEPELEKA ASKARI MAENEO YENYE GHASIA.
No comments:
Post a Comment