September 7, 2009

LUBNA APATWA NA HATIA YA KUVAA SURUALI HADHARANI



MWANDISHI WA KIKE NCHINI SUDAN ANAYETUHUMIWA KWA KOSA LA KUVAA SURUALI HADHARANI, AMEPATIKANA NA HATIA NA KUPIGWA FAINI YA PAUNI 500 ZA SUDAN AMBAZO NI SAWA NA DOLA 209 AU KWENDA JELA MWEZI MMOJA.

MWANAMKE HUYO LUBNA HUSSEIN, AMBAYE NI MFANYAKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AMEKATAA KUILIPA FAINI HIYO AMBAYO IMETOLEWA NA MAHAKAMA YA KHARTOUM NA KUSEMA YUKO TAYARI KWENDA JELA.

AWALI LUBNA AMEKUWA ANAKABILIWA NA ADHABU YA KUCHAPWA VIBOKO 40 KAMA ATAPATIKANA NA HATIA YA KUVAA SURUALI HADHARANI.
LUBNA, AMESHITAKIWA KWA KOSA HILO CHINI YA SHERIA YA KIISLAMU NCHINI SUDAN, BAADA YA KUKAMATWA JULAI, MWAKA HUU PAMOJA NA WANAWAKE WENGINE 12 WALIOKUWA WAMEVAA SURUALI KATIKA MGAHAWA MJINI KHARTOUM.
WANAWAKE WENGINE 10 WAMESHAADHIBIWA CHINI YA SHERIA HIYO NCHINI SUDAN.

No comments:

Post a Comment