September 8, 2009

LUBNA AACHIWA HURU


MWANDISHI WA KIKE NCHINI SUDAN ANAYETUHUMIWA KWA KOSA LA KUVAA SURUALI HADHARANI, AMEACHIWA HURU BAADA YA KUKAA JELA KWA SIKU MOJA.
MWANAMKE HUYO, LUBNA HUSSEIN AMBAYE NI MFANYAKAZI WA UMOJA WA MATAIFA JANA ALIPATIKANA NA HATIA YA KUVAA SURUALI HADHARANI NA KUPIGWA FAINI YA PAUNI 500 ZA SUDAN AMBAZO NI SAWA NA DOLA 209 AU KWENDA JELA MWEZI MMOJA.
HATA HIVYO, ALIKATAA KUILIPA FAINI HIYO ILIYOTOLEWA NA KUSEMA YUKO TAYARI KWENDA JELA. AWALI LUBNA ALIKUWA ANAKABILIWA NA ADHABU YA KUCHAPWA VIBOKO 40 PINDI AKIPATIKANA NA HATIA

No comments:

Post a Comment