
Kesi inayomkabili mwandishi wa habari mwanamke wa Sudan Lubna Ahmed al-Hussein inatarajiwa kusikilizwa hii leo. Mwanamke huyo anayekabiliwa na mashitaka ya kuvaa suruali hadharani atahukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 40, endapo atapatikana na hatia.
Lubna, alishitakiwa kwa kosa hilo chini ya sheria ya Kiislamu nchini Sudan, baada ya kukamatwa Julai, mwaka huu pamoja na wanawake wengine 12 waliokuwa wamevaa suruali katika mgahawa mjini Khartoum.
Mwanamke huyo anafikishwa tena mahakamani ili kubaini iwapo ana kinga ya kidiplomasia dhidi ya mashtaka yanayomkabili. Wanawake wengine 10 wameshaadhibiwa chini ya sheria hiyo nchini Sudan.
Ijumaa iliyopita, Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International liliitaka serikali ya Sudan kufuta mashitaka dhidi ya mwanamke huyo, likisema kuwa sheria hiyo inayohalalisha mwanamke kuchapwa viboko kwa kuvaa suruali ambazo si za heshima, inapaswa kubadilishwa.
No comments:
Post a Comment