June 4, 2009

Obama Aihutubia nchi ya Misri


Rais wa Marekani Barack Obama ametoa hotuba yake muhimu katika chuo kikuu mjini Cairo ambako ameahidi kujaribu kuleta maelewano katika uhusiano baina ya Marekani na ulimwengu wa Kiislamu.


Obama amesema kuwa kundi dogo la Waislamu wenye msimamo mkali limesambaza aina isoyokuwa ya kweli ya Uislamu pamoja na hofu, na ameahidi kuondoa mtengano.

Hotuba hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ilitangazwa katika mtandao wa internet kupitia tovuti ya Twitter, Facebook na MySpace, katika juhudi za kuwafikia wengi wa Waislamu wapatao bilioni 1.5 duniani kote.


Rais Obama yuko katika ziara yake ya kwanza katika mataifa ya Kiarabu tangu kuingia kwake madarakani.

Baadaye atakwenda nchini Ujerumani na Ufaransa katika kumbukumbu ya majeshi ya Marekani kuingia katika vita vikuu vya pili vya dunia.

No comments:

Post a Comment