Serikali ya Gabon imesema kuwa mwili wa rais Omar Bongo Ondimba utarejeshwa nyumbani kutoka Hispania siku ya Alhamis, siku moja kabla ya ilivyopangwa.
Kifo cha rais Bongo mwenye umri wa miaka 73 kilitangazwa na waziri mkuu Jean-Eyeghe Ndong siku ya Jumatatu mjini Barcelona, mji ambao rais huyo amekuwa akipatiwa matibabu tangu mapema May katika hospitali ya binafsi kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo.
Ujumbe wa Gabon unajitayarisha kutoa heshima zao rasmi kwa mwili wa rais Bongo mjini Barcelona kabla ya hatua rasmi za mazishi kufanyika nchini Gabon, ambapo zinatarajiwa kufanyika Ijumaa hadi Jumatatu wiki ijayo.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Hispania imethibitisha kuwa tukio hilo rasmi litafanyika siku ya Alhamis asubuhi mjini Barcelona.
Wakati huo huo serikali ya Gabon itaiomba mahakama kuu nchini humo kumthibitisha seneta Rose Francine Rogombe kuwa kiongozi wa mpito wa Gabon baada ya kifo cha rais Bongo.
No comments:
Post a Comment