Jeshi la wanamaji la Brazil, leo, limepata maiti zingine tatu kutoka kwa ile ndege ya Air France ilioanguka wiki moja iliyopita katika bahari ya Atlantic. Jana kundi linalofanya shughuli ya msako katika eneo la ajali hiyo lilipata maiti za wanaume wawili pamoja na mabaki ya ndege ikiwa ni pamoja na kiti kilichokuwa na nambari ambayo inawiana na zile za ndege hiyo nambari A 447. Idadi ya maiti zilizopatikana hadi kufikia sasa ni maiti tano.
Maafisa nchini Brazil wamesema wanaendelea na msako wao, kilomita 600 mwa pwani ya Brazil, kujaribu kupata maiti zingine. Maafisa wa Ufaransa wanaoendesha msako wa kukitafuta kisanduku cheusi cha kurekodia mawasiliano, wamesema ndege hiyo iliyokua njiani kuelekea mjini Paris kutoka Rio de Janiero ikiwa na abiria 228, ilipata matatizo kadhaa ya kimitambo muda mfupi kabla ya kuanguka.

No comments:
Post a Comment