June 9, 2009

NDUGU WATOA WITO KUACHIWA KWA WAANDISHI

NDUGU WA WAANDISHI HABARI WAWILI WA MAREKANI AMBAO WAMEHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 12 NA KAZI NGUMU WANATOA WITO KWA KOREA YA KASKAZINI KUONESHA HURUMA NA KUWAACHIA WAANDISHI HAO KWA MISINGI YA KIBINADAMU.
WADADISI WA MAMBO WANASEMA KUWA KOREA YA KASKAZINI INATUMIA WAANDISHI HAO KAMA KARATA YA KUWEZA KUFANYA MAJADILIANO ILI MAREKANI IWEZE KURIDHIA.
PIA KUONGEZA HALI YA WASI WASI KATIKA RASI YA KOREA NI PAMOJA NA MATAMSHI MAKALI YANAYOTOKA KATIKA SERIKALI YA KOREA YA KASKAZINI.
KOREA YA KASKAZINI IMEAPA KUTUMIA SILAHA ZAKE ZA KINUKLIA IWAPO UHURU WAKE UTAKUWA HATARINI.
NI MARA YA KWANZA KWA KOREA YA KASKAZINI KUTUMIA NENO MASHAMBULIZI KUHUSIANA NA SILAHA ZAKE ZA KINUKLIA.

No comments:

Post a Comment