August 16, 2012

KLABU ZA LIGI KUU UGANDA KUTIA KIBINDONI MILLIONI 55 KILA MMOJA



KLABU ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU SOKA NCHINI UGANDA (USL) NA KUFANYA MAKUBALIANO YA UDHAMINI ZITAPOKEA KITITA CHA SHILINGI MILLION 55 KILA MMOJA KATIKA MSIMU WA LIGI 2012/2013 WA BELL SUPER LIGI.

FEDHA HIZO AMBAZO ZIMEONGEZEKA KWA KIWANGO CHA SHILINGI MILIONI TANO, NI SEHEMU YA MKATABA WA MIAKA MITANO NA TELEVISHENI YA SUPERSPORT INTERNATIONAL AMBAO NI WASHIRIKA WA UGANDA SUPER LIGI.

KWA MUJIBU WA MKURUGENZI MTENDAJI WA (UGANDA SUPER LIGI) JIMMY EBIL SSEGAWA VILABU AMBAVYO VIMESAINI NA WADHAMINI (BELL LAGER NA SUPERSPORT INTERNATIONAL) VIMEANZA KUPOKEA VIFAA VYAO VYA MZUNGUKO WA KWANZA PAMOJA NA FEDHA TASLIM SHILINGI MILLION 20, HADI 35,  JEZI ZA MECHI KWA NYUMBANI NA UGENINI, MIPIRA 15, PAMOJA BOX 60 ZA MAJI.

KLABU AMBAZO HAZIJAFANYA HIVYO NI VICTORS FC, SIMBA FC, EXPRESS FC, URA FC, MASAKA LC, SC VILLA, KCC FC NA POLICE FC.
MSIMU ULIOPITA SUPERSPORT INTERNATIONAL ILIONESHA MECHI 27, HIVYO MSIMU HUU MPYA WA (2012/13) ITATANGAZA MICHEZO 55 LIVE.

No comments:

Post a Comment