NEW ZEALAND IMEKUBALI KICHAPO CHA MABAO 2-0 KUTOKA KWA VIJANA WA KOCHA MARCIO MAXIMO BAADA YA KUWA WA KWANZA KUPATA BAO LA KUNGOZA KATIKA KIPINDI CHA KWANZA KWENYE MCHEZO WA KIMATAIFA WA KIRAFIKI ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA, JANA JIJINI DAR ES SALAAM.
KATIKA MCHEZO HUO ULIOANZA SAA MOJA ZA USIKU STARS WALIPATA MABAO YAO YOTE KATIKA KIPINDI CHA PILI NA KUONYESHA KIWANGO CHA JUU KILICHOWAPA WAKATI MGUMU WAPINZANI WAO NEW ZEALAND.
ALL WHITES WALIANZA KULIONA LANGO LA STARS DAKIKA YA 10 YA MCHEZO BAADA YA SHANE SMELTZ KUJAZA WAVUNI MKWAJU SAFI WA PENALTI. MCHEZAJI WA STARS, SHAABAN NDITI NDIYE ALIYESABABISHA ADHABU HIYO YA PENALTI WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUONDOA HATARI KWENYE LANGO LAKE, NA KUJIKUTA AKINAWA MPIRA HIVYO, MWAMUZI ODEN MBAGA KUAMURU IPIGWE PENALTI AMBAYO KIPA JUMA DIHILE ALISHINDWA KUIOKOA. BAADA YA BAO HILO STARS WALIJITAHIDI KUTAFUTA BAO LA KUSAWAZISHA NA KUELEKEZA MASHAMBULIZI KWENYE LANGO LA WAPINZANI WAO, LAKINI HAWAKUONEKANA KUWA MAKINI KATIKA KUMALIZIA NAFASI KADHAA WALIZOPATA HUKU WACHEZAJI WAKE MRISHO NGASA, NIZAR KHALFAN , JERRY TEGETE, HENRY JOSEPH NA KIGI MAKASI WAKIONANA VYEMA, LAKINI WALINZI WA NEW ZEALAND WALIKUWA MAKINI KUONDOSHA HATARI HIZO. KIPINDI CHA PILI TIMU ZOTE ZILIINGIA UWANJANI KWA KASI HUKU STARS WAKIFANYA MABADILIKO YA MAPEMA WAKIMTOA KHALFAN NA NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA MWINYI KAZIMOTO. MABADILIKO AMBAYO YALILETA UHAI ZAIDI NA KUPATA BAO LA KUSAWAZISHA KATIKA DAKIKA YA 56 PALE TEGETE ALIPOMALIZIA KWA KICHWA SHUTI KALI LA MRISHO NGASA AMBAYE ALIPOKEA PASI SAFI YA HENRY JOSEPH.
BAADA YA BAO HILO STARS WALIZIDISHA MASHAMBULIZI NA HASA BAADA YA KUWAINGIZA MUSSA HASSAN ‘MGOSI’, JOHN BOCCO NA NURDIN BAKARI BADALA YA KIGI MAKASI, TEGETE NA NDITI MABADILIKO YALILETA UHAI ZAIDI KWA STARS NA KUENDELEA KUONYESHA KANDANDA LA HALI YA JUU. WALIMPA SIFA KOCHA WAO MAXIMO AMBAYE HIVI KARIBUNI ALIJIKUTA AKIZOMEWA NA MASHABIKI WENYE HASIRA KWENYE UWANJA HUO BAADA YA TIMU YAKE KULALA KWA MABAO 2-0 DHIDI YA MABINGWA WA AFRIKA KATIKA MICHUANO YA WACHEZAJI WA LIGI ZA NDANI (CHAN) JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO. MGOSI ALIAMBAA NA MPIRA KATIKA DAKIKA ZA MAJERUHI BAADA YA KUMTOKA DAVID MULIGAN NA KUMPA PASI SAFI KAZIMOTO ALIYEMPIMA KIPA WA ALL WHITES, PATSON NA KUACHIA SHUTI LILILOKWENDA MOJA KWA MOJA WAVUNI NA KUIPATIA STARS BAO LA USHINDI LILILOAMSHA SHANGWE KWA MASHABIKI WA STARS NA KOCHA WAO MARCIO MAXIMO ALIYEKUWA AKIRUKARUKA KWA FURAHA.

No comments:
Post a Comment