June 3, 2009

BRAZIL YATHIBITISHA KUPATIKANA KWA MABAKI YA AIR FRANCE

BRAZIL IMETHIBITISHA KWAMBA MABAKI YA NDEGE YALIYOPATIKANA KWENYE BAHARI YA ATLANTIC NI YA NDEGE YA SHIRIKA LA UFARANSA ILIYOPOTEA WAKATI WA DHORUBA KALI SIKU YA JUMATATU.
WAZIRI WA ULINZI WA BRAZIL, NELSON JOBIM, AMESEMA HAKUNA SHAKA KWAMBA MABAKI HAYO NI YA NDEGE YA SHIRIKA LA AIR FRANCE AINA YA AIRBUS 330. WAZIRI HUYO AMEWAAMBIA WAANDISHI WA HABARI KWAMBA ITAKUWA VIGUMU KUKIPATA KIFAA CHA KUREKODIA SAUTI NA DATA KWA SABABU YA KIMA CHA MAJI AMBAKO MABAKI HAYO YAMEPATIKANA.
BRAZIL IMETANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA KUWAKUMBUKA ABIRIA WOTE 228 WALIOKUWA KWENYE NDEGE HIYO ILIYOTOKEA RIO DE JANEIRO IKIELEKEA PARIS UFARANSA, AMBAO INAAMINIWA WAMEKUFA KATIKA AJALI HIYO. WAJERUMANI 26 NI MIONGONI MWA ABIRIA HAO.
WAKATI HUO HUO, KANSELA WA UJERUMANI, ANGELA MERKEL, AMETOA RISALA ZA RAMBIRAMBI KWA JAMII ZA WAHANGA, AKISEMA AMESHTUSHWA NA AJALI HIYO. UFARANSA ITAONGOZA UCHUNGUZI KUTAFUTA CHANZO CHA AJALI HIYO.

No comments:

Post a Comment