May 26, 2009

NANI KUIBUKA MBABE STADIO OLIMPICO






BAADA YA KUSUBILIA KWA MUDA MREFU SASA KITENDAWILI KITATATULIWA HIYO KESHO MAJIRA YA SAA NNE USIKU KATIKA KIWANJA CHA STADIO OLIMPICO HUKO ROME ITALIA KWA MWAKA HUU WA 2009.

NI KATIKA FAINALI YA CLUB BINGWA ULAYA AMA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KATI YA FC BARCELONA NA MANCHESTER UNITED FC. MECHI HIYO AMBAYO IMETABIRIWA KUWA KALI NA YA KUSISIMUA, KWANI WADAU WA SOKA WENGI WANADAI KWAMBA HUENDA KOMBE HILO LIKABAKI MANCHESTER UNITED KUTOKANA NA TIMU HIYO KUWA TISHIO KATIKA FAINALI HIZO.

IKUMBUKWE YA KWAMBA CLUB YA MANCHESTER UNITED ITAMKOSA MCHEZAJI MAHIRI KATIKA NAFASI YA KATI DAREN FRETCHER AMBAYE ALIZAWADIWA KADI NYEKUNDU KATIKA MECHI YA NUSU FAINALI KATI YAO NA ARSENAL, UPANDE WA BARCELONA WATAMKOSA MBRAZIL DAN ALVES.

WAKIONGEA KWA NYAKATI TOFAUTI MAKOCHA WA TIMU HIZO WAMEONEKANA KUTOKUWA NA WASI WOWOTE NA KUONYESHA KUWA TIM,U ZAO HIZO ZIMEJAPANGA VILIVYO NA ISITOSHE WOTE WAMEKWISHATWAA UBINGWA WA LIGI KUU NCHINI MWAO KWA KILA TIMU.
AIDHA MWAMUZI KATIKA MECHI HIYO ATAKUWA NI MASSIMO BUSACCA KUTOKA USUIZ NA MSAIDIZI WAKE ATAKUWA NI MATHIAS ARNET NAYE PIA KUTOKA SUIZ, WENGINE NI KATIKA BENCH LA UFUNDI KWA UPANDE HUO NI CLAUDIO CIRCHETTA KUTOKA USUIZ NA MSIMAMIZI WA UEFA JIM STJERNE HANSEN KUTOKA DENMARK PAMOJA NA MSIMIZI WA MAREFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA BARANI ULAYA MARC BATTA KUTOKA UFARANSA.

WAKATI HUO FAINALI YA KOMBE LA FA NAYO INATEGEMEWA KUCHEZWA MEI 30 HUKO NCHINI UINGEREZA KATI YA CHELSEA NA EVERTON MWEZI HUU.

No comments:

Post a Comment