Huyu ndiye Mmanga Pandu a.k.a Ras Midude kutoka Zanzibar, Tanzania.
Msanii Khalifa Mmanga Pandu, huyu ni kijana ambaye miaka ya 1999 mpaka mwaka 2006 alikuwa akijishugulisha na kazi za muziki wa kufokafoka almaarufu hip hop.
lakini kumbe chanzo hicho cha usanii kilikuwa kikimpatia nafasi ya kupata uzoefu katika kufanya mazoezi ya kutangaza, na mnamo mwaka 2008 ndipo alipoibuka rasmi na kuwa bonge la mtangazaji katika vituo vya redio mbalimbali hasa kile cha Chuchu Fm cha Zanzibar ambacho jamaa huyu baada ya kuongea naye maneno mawili mattu naye ,
aliweza kusema kazi ya utangazaji aliipenda tangu akiwa mdogo hivyo hashangai kuwa presnter hii sasa, na ni kazi ambayo inampatia kipato chake halali.
No comments:
Post a Comment