September 26, 2014

BENTEKE KURUDI UWANJANI HIVI KARIBUNI


Bosi wa Villa Paul Lambert ameweka wazi kuwa mshambuliaji wake Christian Benteke huenda akajumuika kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Manchester City  October 4.
Benteke aligonga vichwa vya habari nchini Uigereza kufuatia kufunga magoli 23 katika mashindano yote kwa mara ya kwanza akiichezea Villa, na licha ya kukabiliwa na majeruhi msimu uliopita, lakini alifunga magoli 11.
Kurudi kwake uwanjani kutaongeza ari ya kikosi cha Villa na kocha Lambert anasema Benteke anaendelea vizuri, na tamtumia lakini kwa tahadhari kubwa.
Villa inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu England baada ya kufanikiwa kushinda mechi tatu mfululizo katika michezo mitano ambayo timu hiyo imekwishacheza.

No comments:

Post a Comment