September 26, 2014

11 WA BAFANA BAFANA DHIDI YA KONGO BRAZAVILLE
Kocha wa Bafana Bafana Ephraim Mashaba ametangaza kikosi kitakachokabiliana na Congo Brazzaville kwenye mchezo wa kuwania AFCON 2015 utakaopigwa mwezi ujao.
Kikosi hicho kimetangazwa katika makao makuu ya ofisi za chama cha soka nchini humo zilizo mjini Johannesburg hii leo.
Mashaba na kikosi chake watasafiri kwa mara ya kwanza kuelekea mjini Pointe Noire Brazzaville kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa October 11 na kurudiana na Congo October 15 mjini Polokwane.
Bafana Bafana inakamata nafasi ya pili mwa A, nyuma ya Congo baada kushinda bao 3-0 dhidi ya Sudan na kutoka sare tasa na Nigeria mjini Cape Town mwezi uliopita.
Kikosi cha Bafana Bafana:
Makipa:                   

Senzo Meyiwa, Darren Keet, Duimisani Msibi
Mabeki:
Anele Ngcongca, Ayabulela Magqwaka, Sibusiso Khumalo, Thulani Hlatshwayo, Kwanda Mngonyama, Erick Mathoho, Thabo Matlaba, Rivaldo Coetzee, Tefu Mashamaite
Viungo:
Themba Zwane, Sibusiso Vilakazi, Oupa Manyisa, Andile Jali, Dean Furman, Thulani Serero, Mandla Masango, Keagan Dolly, Reneilwe Letsholonyane,
Washambuliaji:  
Tokelo Rantie, Bongani Ndulula, Kermit Erasmus, Fagrie Lakay

No comments:

Post a Comment