August 28, 2012

Tusker announce Shs 1.12 Billion CECAFA Sponsorship
KAMPUNI YA BIA YA EAST AFRICA BREWERIES, KUPITIA BIA YAO YA TUSKER, ASUBUHI YA LEO WAMEKABIDHI HUNDI YA SHILINGI ZA KENYA MILLION 36, (SAWA NA DOLA ZA KIMAREKANI LAKI NNE NA HAMSINI ELFU, NA NI TAKRIBANI BILLIONI 1.12 KWA SHILINGI YA UGANDA ) IKIWA NI SEHEMU YA UDHAMINI WA MICHUANO YA MWAKA HUU YA TUSKER’S CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP.

KATIKA  HAFLA YA MAKABIDHIANO HAYO, PIA KUMETANGAZWA TAREHE YA KUANZA KWA MICHUANO HIYO, AMBAYO NI TAREHE 24 MWEZI WA NOVEMBA NA KUMALIZIKA DESEMBA 8, HUKU SAFARI HII UDHAMINI HUO UKIONGEZEKA KWA ASILIMIA TANO ZAIDI YA UDHAMINI WA MASHINDANO YALIYOPITA.

AKIKABIDHI HUNDI HIYO, MKURUGENZI MASOKO WA (EABL ) LEMMY MUTAHI, AMESEMA KUWA LENGO LA KAMPUNI HIYO NI KUTOA MSAADA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KUHAKIKISHA KWAMBA UKANDA HUU WA MASHARIKI UNATOA TIMU MWAKILISHI KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014 NCHINI BRAZIL.

NAYE KATIBU WA MKUU WA CECAFA, NICOLAS MUSONYE, ALIEONDOKA LEO ASUBUHI NCHINI KENYA KUELEKEA MJINI KAMPALA, AMESEMA KUWA UDHIMINI HUO UTATOSHA KWA TIMU SHIRIKI KUPATA MAHITAJI YOTE MUHIMU.

KATIKA FEDHA ZA UDHAMINI HUO, JUMLA YA DOLA ELFU 60.000 ZIMETENGWA KWA AJILI YA ZAWADI KWA WASHINDI, AMBAPO MSHINDI WA KWANZA ATAJINYAKULIA DOLA ELFU THELATHINI, WA PILI DOLA ELFU ISHIRINI, NA WA TATU ATAPATA DOLA EFLU KUMI, NA MICHEZO YOTE ITAKUWA IKIONYESHWA LIVE NA SUPERSPORT.

SHIRIKISHO LA SOKA UGANDA (FUFA) TAYARI LIMESHAUNDA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MIPANGO YOTE NA MAANDALIZI YA MICHUANO HIYO.

BAADA YA HAFLA HIYO MUSONYE ALIPATA NAFASI YA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA MICHEZO WA UGANDA CHARLES BAKABULINDI OFISINI KWAKE MJINI KAMPALA NA WAZIRI HUYO KUAHIDI KUTOA USHIRIKIANO ILI KUHAKIKISHA FUFA PAMOJA NA CECAFA WANAANDAA MICHUANO HIYO KWA MAFANIKIO.by www.michezoafrika.com

No comments:

Post a Comment