August 28, 2012

EAGLE WINGS RETURN HOME WITH REGIONAL TITLE


KAMA WALIVYOAHIDI TOKA AWALI, MABINGWA WA KIKAPU NCHINI KENYA, TIMU YA WANAWAKE YA EAGLE WINGS JANA USIKU IMEREJEA NYUMBANI KIFUA MBELE, BAADA YA KUWATANDIKA NDUGU ZAO TIMU YA MAMLAKA YA BANDARI (KPA) NA KUTWAA TAJI LA MICHUANO YA KIKAPU YA KANDA YA TANO KWA MWAKA 2012.

WAKIWA NA KOMBE HILO, EAGLE WINGS SASA WAMEPATA TIKETI YA KUWA TIMU PEKEE KUTOKA KENYA ITAKAYOWAKILISHA KWENYE MASHINDANO YA VILABU BINGWA AFRICA, FIBA  YATAKAYOFANYIKA NCHINI IVORY COAST BAADAYE MWEZI OKTOBA.

EAGLE WINGS ILIWABWAGA WAPINZANI WAO WA JADI KPA, KATIKA FAINALI ILIOPIGWA LUGOGO MJINI KAMPALA KWA USHINDI WA VIKAPU 77-54 BAADA YA KUONGOZA KWA ALAMA 31-30 ZA KPA MPAKA HALF TIME.

No comments:

Post a Comment