August 22, 2012

CAMEROON: ETO’O TO REGAINS ARMBAND IN “LION’S DEN”



MSHAMBULIAJI WA KIMATAIFA WA CAMEROON, SAMUEL ETO'O, ALIEKUWA AKITUMIKIA ADHABU YAKE KWA MIEZI NANE, INAYOMALIZIKA MWEZI HUU, AMEITWA NA TIMU YAKE YA TAIFA AMBAPO ATAENDELEA KUWA NAHODHA WA TIMU HIYO.

KWA MUJIBU WA RADIO YA KAMEROUN YA EQUINOX, KOCHA WA TIMU HIYO DENNIS LAVAGNE AMEMUITA ETOO AMBAYE NI  NAHODHA WAKE, ATAKAEIONGOZA TIMU HIYO KATIKA MAANDALIZI YA MCHEZO DHIDI YA CAPE VERDE AMBAO NI WA TATU NA WA MWISHO WA KUWANIA TIKETI YA KUSHIRIKI AFCON 2013.

WIKI MBILI ZILIZOPITA, BAADA YA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA KWENYE MKUTANO WA KWANZA WA MAANDALIZI YA MECHI DHIDI YA CAPE VERDE ULIOFANYIKA WIZARA YA MICHEZO NA ELIMU YA FIZIKIA AGOSTI 21, ILISEMA KUWA TAARIFA YA KUMALIZIKA KWA ADHABU YA ETOO ILITUMWA KWA ETOO PAMOJA NA MWANASHERIA WAKE.

No comments:

Post a Comment