KAMPUNI YA BIA YA EAST AFRICA BREWERIES, KUPITIA BIA
YAO YA TUSKER, ASUBUHI YA LEO WAMEKABIDHI HUNDI YA
SHILINGI ZA KENYA MILLION 36, (SAWA NA DOLA ZA KIMAREKANI LAKI NNE NA HAMSINI ELFU, NA NI TAKRIBANI BILLIONI 1.12 KWA SHILINGI YA UGANDA ) IKIWA NI
SEHEMU YA UDHAMINI WA MICHUANO YA MWAKA HUU YA TUSKER’S CECAFA SENIOR CHALLENGE
CUP.
KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO HAYO, PIA KUMETANGAZWA TAREHE YA KUANZA KWA MICHUANO HIYO, AMBAYO NI TAREHE 24 MWEZI WA NOVEMBA NA KUMALIZIKA DESEMBA 8, HUKU SAFARI HII UDHAMINI HUO UKIONGEZEKA KWA ASILIMIA TANO ZAIDI YA UDHAMINI WA MASHINDANO YALIYOPITA.
AKIKABIDHI HUNDI HIYO, MKURUGENZI MASOKO WA (EABL ) LEMMY MUTAHI, AMESEMA KUWA LENGO LA KAMPUNI HIYO NI KUTOA MSAADA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KUHAKIKISHA KWAMBA UKANDA HUU WA MASHARIKI UNATOA TIMU MWAKILISHI KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2014 NCHINI BRAZIL.

NAYE KATIBU WA MKUU WA CECAFA, NICOLAS MUSONYE, ALIEONDOKA LEO ASUBUHI
NCHINI KENYA KUELEKEA MJINI KAMPALA, AMESEMA KUWA UDHIMINI HUO UTATOSHA KWA
TIMU SHIRIKI KUPATA MAHITAJI YOTE MUHIMU.
KATIKA FEDHA ZA UDHAMINI HUO, JUMLA YA DOLA ELFU 60.000 ZIMETENGWA KWA AJILI YA ZAWADI KWA WASHINDI, AMBAPO MSHINDI WA KWANZA ATAJINYAKULIA DOLA ELFU THELATHINI, WA PILI DOLA ELFU ISHIRINI, NA WA TATU ATAPATA DOLA EFLU KUMI, NA MICHEZO YOTE ITAKUWA IKIONYESHWA LIVE NA SUPERSPORT.

SHIRIKISHO LA SOKA UGANDA (FUFA) TAYARI
LIMESHAUNDA KAMATI YA KUSHUGHULIKIA MIPANGO YOTE NA MAANDALIZI YA MICHUANO
HIYO.
BAADA YA HAFLA HIYO MUSONYE ALIPATA NAFASI YA KUZUNGUMZA NA WAZIRI WA
MICHEZO WA UGANDA CHARLES BAKABULINDI OFISINI KWAKE MJINI KAMPALA NA WAZIRI HUYO
KUAHIDI KUTOA USHIRIKIANO ILI KUHAKIKISHA FUFA PAMOJA NA CECAFA
WANAANDAA MICHUANO HIYO KWA MAFANIKIO.
by www.michezoafrika.com
No comments:
Post a Comment