WIZARA YA VIJANA NA MICHEZO NCHINI TUNISIA
IMEAMUA KUZUIA BAADHI YA MICHEZO YA RAUNDI
YA SITA LIGI YA TAIFA ILIYOSALIA KUCHEZWA MILANGO IKIWA IMEFUNGWA KUFUATIA VURUGU ZILIZOJITOKEZA KATIKA YA MECHI
YA JUMAPILI YA KLABU BINGWA KATI YA ETOILE DU SAHEL NA ESPERANCE, MPAMBANO
ULIOMALIZIKA KWA ESPERENCE KUSHINDA BAO 2-0.
KUFUATIA VURUGU HIZO, MSHAURI WA WAZIRI WA MICHEZO NCHINI TUNISIA, JALEL
TEKAYA AMESEMA KUWA WIZARA YA MICHEZO
NA VIJANA IMEAMUA KUHITIMISHA MSIMU WA LIGI SOKA YA TAIFA NCHINI HUMO KUCHEZWA BILA UWEPO WA UMMA KATIKA VIWANJA MBALIMBALI ILI
KUEPUKA MATATIZO ZAIDI.
MASHABIKI WA TIMU MWENYEJI AMBAYO NI ES SAHEL, WALIVAMIA
UWANJA WAKIPINGA MAAMUZI YA REFA JUU YA MCHEZAJI
ALIEKUWA AMEOTEA, NA KUFANYA MCHEZO HUO USIMAME KWA
DAKIKA 12.
VURUGU ZA MASHABIKI HAO ZILIZIDI KUPAMBA MOTO BAADA YA
MCHEZAJI RAIA WA CAMEROON YANICK N'JENG KUPIGA BAO LA PILI, BAADA YA MAPUMZIKO,
HIVYO KUIBUA HISIA KALI KWA MASHABIKI WALIOKUSHUKA UWANJANI NA KUANZA
KUMBUGUDHI REFA NA MALINESMEN WAKE, KITU AMBACHO KILIWALAZIMU ASKARI WA USALAMA
KUFYATUA MABOMU YA MACHOZI NA KUPELEKEA MCHEZO HUO KUVUNJIKA DK YA 71.
No comments:
Post a Comment