MCHEZAJI SOKA WA KIMATAIFA RAIA WA SENEGAL MUSA KONATE
AMESAINI MKATABA WA MIAKA MITATU WA KUICHEZEA KLABU YA FC KRASNODAR INAYOSHIRIKI
LIGI KUU SOKA NCHINI URUSI, AKITOKEA MACCABI TEL AVIV YA ISRAEL, BAADA YA
KUITUMIKIA KLABU HIYO KWA MSIMU WA MWAKA 2011 AKITOKEA KLABU YA VIJANA YA
SENEGAL YA TOURE KUNDA.
KULINGANA NA SHIRIKA LA HABARI LA SENEGAL (APS), MSHAMBULIAJI
HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 19, JUMATANO WIKI HII ALIFAULU
VIPIMO VYA MJINI TEL AVIV ULIOFANYWA NA MADAKTARI
WALIOKUWA WAKIIWAKILISHA KLABU HIYO URUSI.
KATIKA UHAMISHO HUO HAKUNA MAELEZO
YOYOTE YA KIFEDHA JUU YA
MKATABA WAKE, LAKINI
MBALI NA UHAMISHO HUO PIA MCHEZAJI HUYO KAPEWA MWAKA MMOJA WA ZIADA.
KLABU HIYO ILIMALIZA NAFASI YA TISA KWENYE MSIMAMO WA LIGI KUU URUSI.
KONATE ALIKUWA WA PILI KWA UFUNGAJI
MAGOLI KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI
2012 JIJINI LONDON KATIKA SOKA LA WANAUME, AKIFUNGA BAO TANO KATI
YA SITA KWA TIMU YAKE.
SENEGAL WALITUPWA NJE YA MASHINDANO KATIKA HATUA YA ROBO FAINALI NA HATIMAYE, MEXICO KUIBUKA MABINGWA KWA
USHINDI WA BAO 4-2.
No comments:
Post a Comment