SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI UGANDA (FUFA) LIMETEUA KAMATI YA
WATU KUMI AMBAO WATAANZA MCHAKATO WA MAANDALIZI YA MICHUANO YA CECAFA SENIOR
CHALLENGE CUP MAPEMA MWAKA HUU AMBAPO UGANDA NDIO MWENYEJI WA MICHUANO HIYO
ITAKAYOFANYIKA KATIKA UWANJA WA NELSON MANDELA MJINI KAMPALA.
AFISA HABARI WA FUFA RODGERS MULINDWA, AKIZUNGUMZA NA
WANAHABARI AMESEMA SAFARI HII WANATAKA KUANDAA MICHUANO HIYO KATIKA UBORA WA
HALI YA JUU, IKILINGANISHWA NA MWAKA 2008 WALIPOKUWA WENYEJI WA MICHUANO HIYO.
MULINDWA AMEONGEZA KUWA WATAHAKIKISHA WANATOA HUDUMA NZURI
KWA TIMU PAMOJA NA MASAHBIKI, LAKINI KWA SASA WAKO KATIKA MAZUNGUMZO NA
SERIKALI YA UGANDA ILI WAWEZE KUUFANYIA UKARABATI UWANJA WA NAMBOOLE KWA AJILI
YA KUFANIKISHA MICHUANO HIYO.
No comments:
Post a Comment