May 27, 2009

KARIBU ZANZIBAR

Manispaa ya Zanzibar inaundwa na jamii ya watu wenye asili tofauti, baadhi yao wakiwa wanatoka sehemu za kati barani Afrika, Asia na Mashariki ya Kati.
Hali hii imesababisha kuchanganyika kwa mila na jadi za Waafrika pamoja na Waarabu na Waasia kwa karne zote hizi, kubwa lililowaunganisha ikiwa ni biashara.
Wazanzibari wengi ni Waislamu wanaotoka kwenye madhehebu tofauti kama vile Sunni, Shia, Ibaadh au Ahmadiya, japokuwa wengi wao ni Sunni.

Zanzibar ina utajiri mkubwa wa urithi wa utamaduni na utamaduni kwa watu hawa, ni zao la maingiliano kati ya wenyeji wa visiwa hivi na wageni waliofika Zanzibar katika nyakati tofauti na kwa madhumuni mbalimbali. Wageni hawa waliwaathiri sana wenyeji wao katika nyanja za dini, sanaa za mavazi, vyakula na lugha ya Kiswahili.

No comments:

Post a Comment