August 27, 2012

NYOTA WA NBA WAMALIZA ZIARA DAR KWA MAFANIKIO


Nyota wa kikapu Luol Deng wa Chicago Bulls na Hasheem Thabeet wa Oklahoma City Thunder wameendesha mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo chini ya miaka 18.

Mafunzo hayo yalifanyika katika viwanja vya Don Bosco, ijumaa na jumamosi jiji Dar Es Salaam.

Pia mafunzo hayo yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa NBA Afrika ndugu Amadou, Kocha wa NBA na Mkurugenzi wa Ufundi wa NBA Afrika Jobby na Meneja Mkuu na Makamu wa Rais wa timu ya Denver Nuggets ndugu Masai.

Ujio wa nyota hao na vigogo hao NBA ni faraja kubwa kwa kikapu Tanzania na ni matumaini yetu itakuwa ni chachu ya kukuza mchezo huo nchini.

Pia mazungumzo yalifanyika kati ya viongozi wa TBF na NBA kuangalia namna ya NBA kusaidia kuendeleza mchezo wa kikapu nchini na hususani katika maeneo ya miundombinu na kusaidoa kujenga uwezo wa kiufundi kwa makocha wazalendo ili kuwa na maendeleo endelevu katika kikapu.

Wachezaji hao nyota  pamoja na viongozi wa NBA  waliagwa kwa ghalfa maalumu iliyofanyika Hotel ya Sea Cliff  jumamosi usiku ambayo ilihudhuriwa na viongozi wa TBF , Wafadhili CocaCola na wameondoka Dar Es Salaam jana jumapili katika uwanja wa ndege wa Julias Nyerere waliagwa na Makamu wa Rais wa TBF ndg. Magesa, pia walikuwepo  Katibu Mkuu wa TBF ndg. Msoffe na Katibu Msaidizi ndg. Maluwe.

Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa kikaupu Tanzania tunawashukuru wachezaji hao na viongozi wote wa NBA na tunaishukuru sana kampuni ya CocaCola kupitia kinywaji cha SPRITE kwa kudhamini mafunzo hayo.

Phares Magesa
Makamu wa Rais- TBF.

No comments:

Post a Comment