August 24, 2012

MALI SCOUTS SAKO



KOCHA WA MALI PATRICE CARTERON JUMATANO HII ALIKUWA SAINT ETIENNE NCHINI UFARANSA, AKIFUATILIA MAZOEZI YA MCHEZAJI BAKARY SAKO MWENYE UMRI WA MIAKA 24, KUNAKO KITUO CHA ETRAT, AMBAPO MWAKA 201O MCHEZAJI HUYO ALIFANYA VIZURI KATIKA LIGI ONE NCHINI HUMO.

SAKO NI MZALIWA WA UFARANSA, JAPO WAZAZI WAKE NI RAIA WA MALI, KWANI ANAMILIKI HATI YA KUSAFIRIA YA UFARANSA NA AMEKICHEZEA KIKOSI CHA TIMU YA VIJANA WA NCHI HIYO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 21, NA HIVI SASA ANAJIWINDA KUJIUNGA NA TIMU YA WAKUBWA.

KOCHA CARTERON NIA NA MADHUMUNI YA SAFARI YAKE ILIUKUWA NI KUMSHAWISHI MCHEZAJI HUYO KUREJEA KUKIPIGA NA TIMU YA TAIFA YA MALI, LAKINI MAZUNGUMZO YALIYOFANYIKA BAINA YA PANDE MBILI HIZO BADO YANASUBIRI UAMUZI WA MCHEZAJI MWENYEWE.

TIMU YA TAIFA YA MALI ITACHEZA NA BOTSWANA MCHEZO WAKE WA KWANZA MJINI BAMAKO MAPEMA MWEZI WA TISA KUTAFUTA TIKETI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA AFCON 2013.

No comments:

Post a Comment