Kocha wa Bafana Bafana
Ephraim Mashaba ametangaza kikosi kitakachokabiliana na Congo Brazzaville kwenye
mchezo wa kuwania AFCON 2015 utakaopigwa mwezi ujao.
Kikosi hicho
kimetangazwa katika makao makuu ya ofisi za chama cha soka nchini humo zilizo
mjini Johannesburg hii leo.
Mashaba na kikosi chake
watasafiri kwa mara ya kwanza kuelekea mjini Pointe Noire Brazzaville kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa October
11 na kurudiana na Congo October 15 mjini Polokwane.
Bafana Bafana inakamata
nafasi ya pili mwa A, nyuma ya Congo baada kushinda bao 3-0 dhidi ya Sudan na
kutoka sare tasa na Nigeria mjini Cape Town mwezi uliopita.
Kikosi cha Bafana
Bafana:
Makipa:
Senzo Meyiwa, Darren
Keet, Duimisani Msibi
Mabeki:
Anele Ngcongca,
Ayabulela Magqwaka, Sibusiso Khumalo, Thulani Hlatshwayo, Kwanda Mngonyama,
Erick Mathoho, Thabo Matlaba, Rivaldo Coetzee, Tefu Mashamaite
Viungo:
Themba Zwane, Sibusiso
Vilakazi, Oupa Manyisa, Andile Jali, Dean Furman, Thulani Serero, Mandla
Masango, Keagan Dolly, Reneilwe Letsholonyane,
Washambuliaji:
Tokelo Rantie, Bongani
Ndulula, Kermit Erasmus, Fagrie Lakay